Recent Articles

Sunday, May 20, 2018

Picha za matukio ya Usiku wa Hip Hop Takatifu na Yesu Okoa Mitaa Ministry (YOM) !!


Usiku wa Hip Hop Takatifu  ulioandaliwa na huduma ya Yesu Okoa Mitaa  (YOM) wafana .Usiku huo uliokua na lengo kutangaza Injili kwa njia ya muziki wa aina ya kufoka-foka ujulikanao kama hip hop ulihudhuriwa na wageni kadhaa kutoka madhehebu tofauti jijini Dar es Salaam .Historia inaonyesha  muziki wa hip hop ulichukua kasi kuanzia miaka ya 1980 hata hivyo haukupokelewa vizuri sana makanisani nchini Tanzania kama njia ya kuhubiri injili kwa vijana kama ambavyo ipo hivi sasa .

" Kuna wachungaji walitupinga sana na kutuona tunapotosha vijana " alinukuliwa ndugu David Robert Mwamsojo nguli wa muziki wa injili Tanzania ambaye alikua mgeni rasmi katika usiku huo .
David  alitamba sana miaka ya 2000 kupitia nyimbo zake .Wimbo wa Bwana atafanya njia na Kiganjani pa Mungu uligusa wengi na kubadilisha maisha ya vijana akiwemo Rapper Peter Banzi ambaye usiku huo alikabidhiwa tuzo ya heshima pamoja na waimbaji wengine wa Gospel hip hop kufuatia mchango wao katika kuuendeleza kupitia injili .Baadhi ya waimbaji wengine waliopewa tuzo usiku huo alikua mwimbaji Emmanuel Mbasha , David Robert ,Meshack , Baltazary Morefire, Kuhani Zangina , Gospo Media ,Hossein Gabriel na Dj Supremacy kutoka  Praise Power radio .
Kwa mujibu wa President wa YOM ministry rapper Rungu la Yesu alimwelezea mgeni rasmi kupitia risala yake jinsi muziki wa gospel hip hop unavyogusa maisha ya wengi kwa sasa hususan vijana na wengi kuweza kuamini injili pamoja na kubadilishwa maisha yao akiwemo rapper maarufu wa kundi la hard blasters - Fanani ambaye ameamua kumfuata Yesu hivi karibuni .


Picha zote na taarifa kwa hisani ya Erasmus Kamugisha kutokea EK Studios . Event hosted by Christ Worship Center  pamoja na Praise Power Radio .

18.05.2018

Picha zaidi BONYEZA HAPA .

Friday, April 13, 2018

Noel + Julieth Special Day - EK StudiosMUA : Irene Beauty Point

Stylist: Erasmus K

EK Studios

Tuesday, August 22, 2017

Tanzania Weddings - love story#Ezekiel and Matulo - August 2017 by EK Studios